Software na Ushauri wa TEHAMA kwa Biashara Yako
Kila huduma imeundwa kutatua tatizo maalum la biashara yako, kuanzia malipo hadi usimamizi wa mauzo na inventory.
Mobile Apps
Tunatengeneza applications za Android na iOS zinazoendana na mfumo wa biashara yako, iwe ni app ya wateja, app ya ndani ya kampuni, au huduma ya mtandaoni.
- Apps za biashara, huduma, au marketplace
- Muunganiko na mifumo yako mingine (payments, SMS, database)
- Usanifu rahisi kutumia kwa Kiswahili au Kiingereza
- Msaada wa matengenezo baada ya kusimika
Mifumo ya Malipo
Kufuatia matakwa ya sasa ya kisheria kuhusu malipo yasiyo ya cash kwa baadhi ya miamala, tunakusaidia kuchagua na kusimika mfumo sahihi wa malipo kwa aina ya biashara yako.
- Biashara ndogo (mfano cafe/restaurant): mifumo rahisi ya Lipa Namba
- Biashara kubwa: muunganiko na payment gateways zilizosajiliwa BOT (mfano Azampesa, Selcom)
- Control namba kwa kila mteja na invoice ya order
- Ushauri wa mfumo unaofaa zaidi kulingana na ukubwa wa biashara yako
Bulk SMS
Mfumo wa kutuma ujumbe kwa wingi kwa wateja wako, matangazo ya bidhaa, arifa za malipo, au taarifa muhimu za biashara moja kwa moja kwa simu za wateja.
- Utumaji wa SMS kwa wingi kwa wateja wote au kikundi maalum
- Ujumbe wa kiotomatiki (mfano arifa ya malipo au order)
- Ripoti za ujumbe uliotumwa na kufika
Mauzo & Inventory (POS)
Mfumo wa kusimamia mauzo, hisa (stock), na taarifa za kifedha za biashara yako kwa wakati halisi, kutoka dukani hadi maghala mengi.
- Usajili wa bidhaa na ufuatiliaji wa stock
- Kumbukumbu za mauzo na ripoti za mapato kwa siku/wiki/mwezi
- Onyo la stock inapokaribia kuisha
- Muunganiko na mfumo wa malipo na risiti za kielektroniki
Ushauri wa TEHAMA
Kwa wale wasiohitaji software mpya bali mwongozo, tunatoa ushauri wa kitaalam kuhusu uchaguzi wa mfumo, usalama wa data, na jinsi ya kudigitize shughuli za biashara.
- Uchambuzi wa mahitaji halisi ya biashara yako
- Ushauri wa uchaguzi kati ya mifumo mbalimbali iliyopo sokoni
- Mpango wa utekelezaji (implementation roadmap)
Huna Uhakika Unahitaji Nini?
Tuma ujumbe WhatsApp ukieleza changamoto ya biashara yako, tutakushauri huduma inayofaa zaidi.