SoftRiver Technologies
Kampuni ya Tanzania inayotengeneza software na kutoa ushauri wa TEHAMA kwa biashara na taasisi zinazotaka kudigitize shughuli zake.
Software Inayolenga Matokeo, Si Maonyesho
SoftRiver Technologies ni jina la biashara lililosajiliwa BRELA (Sole Proprietary). Tunafanya kazi na wamiliki wa biashara ndogo na za kati, taasisi, na watu binafsi wanaotaka kutumia teknolojia kuboresha jinsi wanavyofanya kazi.
Tunachanganya utengenezaji wa software na ushauri wa kitaalam, hivyo hutapata tu mfumo, bali pia mwongozo wa jinsi ya kuutumia vizuri kukuza biashara yako.
- Jina la biashara: SoftRiver Technologies
- Aina: Sole Proprietary (Umiliki wa Mtu Mmoja)
- Usajili: BRELA, Tanzania
- Maeneo ya huduma: Tanzania nzima (mtandaoni)
- Mawasiliano: WhatsApp na Simu
Jinsi Tunavyofanya Kazi
Uwazi
Tunaeleza gharama, muda, na uwezo halisi wa mfumo kabla ya kuanza kazi, hakuna ahadi za uongo.
Ubunifu Unaolenga Wewe
Kila biashara ni tofauti, hivyo tunarekebisha mfumo kulingana na mahitaji yako badala ya kukubandika suluhisho la jumla.
Msaada wa Kudumu
Baada ya kusimika mfumo, tunabaki karibu kwa msaada wa kiufundi na maboresho yajayo.
Tuambie Kuhusu Biashara Yako
Tupigie au tutumie ujumbe WhatsApp, tutaanza na mazungumzo ya bure kuhusu mahitaji yako.